MAANA YA FASIHI
Fasihi ni sanaa ya lugha. Fasihi
hutumia lugha kutoa sanaa mbalimbali katika jamii.
Tanzu za Fasihi
Kuna tanzu mbili kuu za fasihi, na
kila utanzu una vipera vyake: Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi:
1.
Hadithi (Ngano)
- hekaya, mighani, visasili n.k
2.
Nyimbo -
za jandoni, za ndoa, za kazi n.k
3.
Maigizo -
michezo ya kuigiza, ngomezi n.k
4.
Tungo Fupi - methali, vitendawili n.k
1.
Hadithi Fupi - hadithi isiyokuwa ndefu
iliyochapishwa katika mkusanyiko wa hadithi nyingine
2.
Riwaya -
hadithi ndefu iliyochapishwa katika kitabu chake pekee
3.
Tamthilia - mchezo wa kuigiza uliowekwa
kwa maandishi
4.
Ushairi* - mashairi yaliyoandikwa
Tofauti kuu kati ya fasihi simulizi
na fasihi andishi ni kwamba Fasihi Simulizi huwasilishwa kwa njia ya mdomo au
matendo ilhali Fasihi Andishi huwasilishwa kwa njia ya maandishi.
Tanbihi:Ushairi ni kipera cha nyimbo lakini pia mashairi yanaweza kuwa
chini ya Fasihi Andishi, ikiwa yamechapishwa.
Comments
Post a Comment