UMUHIMU WA FASIHI

Umuhimu wa Fasihi Katika Jamii

  • Kuburudisha jamii. Takribani vipera vyote vya fasihi huwa na kusudi la kufurahisha, kutumbuiza na kusisimua hadhira.
  • Kuelimisha. Fasihi hukusudia kuelimisha hadhira kuhusu jamii, mazingira n.k
  • Kudumisha maadili katika jamii kwa kuelekeza, kuonya na kunasihi hadhira jinsi ya kufuata mwelekeo unaokubalika katika jamii.
  • Kuunganisha jamii. Fasihi huleta pamoja watu katika jamii. Kwa mfano, katika nyimbo, miviga, vichekesho.
  • Kukuza lugha. Aghalabu tungo zote za fasihi hutumia lugha. Isitoshe, fasihi hutumia mbinu nyingi za lugha. Wasimulizi na waandishi wa fasihi huhitaji kuwa na ukwasi wa lugha.
  • Kuhifadhi mila, tamaduni na itikadi za jamii. Aghalabu kazi za fasihi (hasahasa Fasihi Simulizi) huambatanishwa na desturi mbalimbali za jamii husika.
  • Kukuza uwezo wa kufikiri. Vipera vingi vya fasihi huwachochea hadhira kufikiri sana ili kupata suluhisho. k.m vitendawili, ngano za mtanziko n.k

Comments

  1. Blog nzur endelea kuweka vitu ili watu wanufaike

    ReplyDelete
  2. Nimeipenda kama mwl wa kiswahili uko vizuri

    ReplyDelete
  3. Nimependa kazi hii sana endelea kuweka vitu zingine yaani watu wasome kwa lugha hii na asanteni.

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

TOFAUTI KATI YA FASIHI SIMULIZI NA ANDISHI

MAANA YA FASIHI