Posts

Showing posts from January, 2018

UMUHIMU WA FASIHI

Umuhimu wa Fasihi Katika Jamii Kuburudisha jamii. Takribani vipera vyote vya fasihi huwa na kusudi la kufurahisha, kutumbuiza na kusisimua hadhira. Kuelimisha. Fasihi hukusudia kuelimisha hadhira kuhusu jamii, mazingira n.k Kudumisha maadili katika jamii kwa kuelekeza, kuonya na kunasihi hadhira jinsi ya kufuata mwelekeo unaokubalika katika jamii. Kuunganisha jamii. Fasihi huleta pamoja watu katika jamii. Kwa mfano, katika nyimbo, miviga, vichekesho. Kukuza lugha. Aghalabu tungo zote za fasihi hutumia lugha. Isitoshe, fasihi hutumia mbinu nyingi za lugha. Wasimulizi na waandishi wa fasihi huhitaji kuwa na ukwasi wa lugha. Kuhifadhi mila, tamaduni na itikadi za jamii. Aghalabu kazi za fasihi (hasahasa Fasihi Simulizi) huambatanishwa na desturi mbalimbali za jamii husika. Kukuza uwezo wa kufikiri. Vipera vingi vya fasihi huwachochea hadhira kufikiri sana ili kupata suluhisho. k.m vitendawili, ngano za mtanziko n.k ...

TOFAUTI KATI YA FASIHI SIMULIZI NA ANDISHI

Tofauti kati ya Fasihi Andishi na Fasihi Simulizi FASIHI SIMULIZI FASIHI ANDISHI 1. Huwasilishwa kwa njia ya mdomo na/au matendo. Huwasilishwa kwa njia ya maandishi 2. Ni mali ya jamii. Kazi andishi ni mali ya mwandishi (na mchapishaji) 3. Msimulizi anaweza kubadilisha sehemu fulani Kitabu kilichoandikwa hakiwezi kubadilishwa 4. Huhifadhiwa akilini Huhifadhiwa vitabuni 5. Kazi simulizi hubadilika na wakati Kazi andishi haibadiliki na wakati 6. Huhitaji msimulizi na hadhira yake wawe mahali pamoja wakati wa masimulizi Msomaji anaweza kusoma kitabu cha hadithi peke yake, mahali popote, wakati wowote 7. Mtu yeyote anaweza kutunga na kusimulia Ni lazima mwandishi na msomaji wawe na uwezo wa kusoma 8. Hutumia wahusika changamano (wanyama, wat...

MAANA YA FASIHI

Image
Fasihi ni sanaa ya lugha. Fasihi hutumia lugha kutoa sanaa mbalimbali katika jamii. Tanzu za Fasihi Kuna tanzu mbili kuu za fasihi, na kila utanzu una vipera vyake:  Fasihi Simulizi  na  Fasihi Andishi : Fasihi Simulizi 1.      Hadithi  (Ngano) - hekaya, mighani, visasili n.k 2.      Nyimbo  - za jandoni, za ndoa, za kazi n.k 3.      Maigizo  - michezo ya kuigiza, ngomezi n.k 4.      Tungo Fupi  - methali, vitendawili n.k Fasihi Andishi 1.      Hadithi Fupi  - hadithi isiyokuwa ndefu iliyochapishwa katika mkusanyiko wa hadithi nyingine 2.      Riwaya  - hadithi ndefu iliyochapishwa katika kitabu chake pekee 3.      Tamthilia  - mchezo wa kuigiza uliowekwa kwa maandishi 4.      Ushairi*  - mashairi yaliyoandikwa Tofauti kuu kati ya fasihi si...

ASILI NA CHIMBUKO LA KISWAHILI

Image
ASILI NA CHIMBUKO LA KISWAHILI Wataalamu wa lugha wameandika kuhusu lugha ya Kiswahili kama lugha ya taifa na lugha rasmi inayokadiriwa kutumiwa na watu wapatao zaidi ya milioni 60 duniani kote.