UMUHIMU WA FASIHI
Umuhimu wa Fasihi Katika Jamii
- Kuburudisha jamii. Takribani vipera
vyote vya fasihi huwa na kusudi la kufurahisha, kutumbuiza na kusisimua
hadhira.
- Kuelimisha. Fasihi hukusudia
kuelimisha hadhira kuhusu jamii, mazingira n.k
- Kudumisha maadili katika jamii kwa
kuelekeza, kuonya na kunasihi hadhira jinsi ya kufuata mwelekeo
unaokubalika katika jamii.
- Kuunganisha jamii. Fasihi huleta
pamoja watu katika jamii. Kwa mfano, katika nyimbo, miviga, vichekesho.
- Kukuza lugha. Aghalabu tungo zote za
fasihi hutumia lugha. Isitoshe, fasihi hutumia mbinu nyingi za lugha.
Wasimulizi na waandishi wa fasihi huhitaji kuwa na ukwasi wa lugha.
- Kuhifadhi mila, tamaduni na itikadi
za jamii. Aghalabu kazi za fasihi (hasahasa Fasihi Simulizi) huambatanishwa
na desturi mbalimbali za jamii husika.
- Kukuza uwezo wa kufikiri. Vipera
vingi vya fasihi huwachochea hadhira kufikiri sana ili kupata suluhisho.
k.m vitendawili, ngano za mtanziko n.k
Blog nzur endelea kuweka vitu ili watu wanufaike
ReplyDeleteNimeipenda kama mwl wa kiswahili uko vizuri
ReplyDeleteNimependa kazi hii sana endelea kuweka vitu zingine yaani watu wasome kwa lugha hii na asanteni.
ReplyDeleteNzuri sana
ReplyDeletekazi hii imenoga
ReplyDelete